Tumia Akili Bandia (AI) kuuza zaidi, kuokoa muda na kuhudumia wateja wako vizuri zaidi. Kwa vitendo, kwenye simu yako, ndani ya saa mbili na nusu.
Kila sehemu ni ya vitendo: unaandika maagizo yako mwenyewe kuhusu biashara yako, na unaondoka na kazi zilizokamilika.
Zana za bure zinazoelewa Kiswahili, kwenye simu yako. Tutazifungua pamoja hatua kwa hatua.
Maelezo ya bidhaa, ujumbe wa kufuatilia wateja na majibu ya "bei ni kubwa" yanayouza.
Ujumbe wa kukaribisha, majibu ya haraka na kujibu malalamiko kwa utulivu.
Mpango wa maudhui wa wiki nzima, maandishi ya picha na mawazo ya video fupi kwa dakika 20.
Nukuu za bei, barua za kiofisi (YAH:) na mapendekezo ya ukurasa mmoja kwa dakika chache.
Taarifa zipi usiweke, jinsi ya kuhakiki ukweli, na kuepuka makosa yanayoaibisha biashara.
Kama unatumia WhatsApp kila siku, unaweza kutumia AI. Warsha hii ni kwa:
Mkurugenzi Mtendaji wa RIC Agency na mwanzilishi wa Shechinah Group. Anajenga mifumo ya AI na WhatsApp inayohudumia biashara na taasisi Tanzania. Mmoja wa Top 100 CEOs of Africa 2026.
Chagua tarehe moja kati ya hizi mbili. Maudhui ni yale yale kwa tarehe zote.
Tuma TZS 35,000 (hadi Jumatatu, 2 Novemba 2026) au TZS 50,000 baada ya hapo, kwenda namba:
Hifadhi ujumbe wa uthibitisho wa M-Pesa.
Bonyeza kitufe hiki, andika jina lako, tarehe uliyochagua na namba ya muamala.
Tunakutumia mwongozo wa "AI kwa Biashara Yako" mara tu tunapothibitisha malipo, na kiungo cha warsha siku moja kabla.
"AI kwa Biashara Yako": kurasa 19, fomula ya agizo zuri, kanuni za usalama na maagizo 100 tayari kutumia.
Warsha hii hii kwa kampuni, kanisa, SACCO au shule yako. Nusu siku, hadi watu 25, mtandaoni au Dar es Salaam, kwa mifano ya kazi yenu.
Biashara yako ijibu wateja saa 24 kwa Kiswahili na Kiingereza, ipokee oda na ikuletee mteja anayehitaji mtu.
Hapana. Simu janja yenye intaneti inatosha. Kompyuta ni nzuri zaidi lakini si lazima.
Hapana. Tunaanza mwanzo kabisa, kwa Kiswahili, na tunafanya kwa vitendo.
Ndiyo. Tunatumia matoleo ya bure. Utaamua mwenyewe baadaye kama unahitaji toleo la kulipia.
Utapata rekodi ya warsha kwa siku 30, au unaweza kuhamia tarehe nyingine. Tujulishe kwa WhatsApp.
Mtandaoni. Siku moja kabla utatumiwa kiungo cha kujiunga kwa WhatsApp. Kinafunguka kwenye simu au kompyuta bila kusakinisha chochote.
Ndiyo. Kwa mafunzo ya timu tunatoa ankara (invoice) ya kulipa benki CRDB. Tuandikie WhatsApp.